Dodoma FM

Mwenyekiti baraza la vyama vya siasa azungumzia kazi ya baraza hilo

15 August 2024, 5:58 pm

Picha ni Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini Tanzania, Juma Ali Khatibu.Picha na George John.

Khatibu amesema kitendo cha kuhudhuria viongozi na wajumbe wa baraza katika tukio hilo ni ishara wapo tayari kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa.

Na Seleman Kodima.
Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini Tanzania, Juma Ali Khatibu amesema kazi kubwa ya baraza hilo ni kuishauri Serikali katika mambo muhimu yanayohusu siasa na wananchi, huku akiishukuru Serikali kwa ushirikiano inaouonyesha.

Khatibu ameyasema hayo leo kwenye hafla iliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) ya kutoa tamko kuhusu uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024.

Picha ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela.Picha na George John.

Tukio hilo limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa, Serikali akiwemo Naibu Msajili wa vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza huku mgeni rasmi akiwa ni Waziri wa Tamisemi, Mohamed Mchengerwa.

Sauti ya Juma Ali Khatibu.

Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela ameahidi kuwa katika uchaguzi ujao wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu watazingatia maadili ya uchaguzi, sheria na taratibu.

Sauti ya Mh.Martine Shigela .