Dodoma FM

Upatikanaji wa maji Vikonje waimarika

5 August 2024, 5:44 pm

Picha ni eneo kilipo kisima cha maji katika eneo hilo la Vikonje.Picha na George John.

Wanasema mwanzoni walikuwa wanapata maji yasiyo salama kutoka vyanzo visivyosahihi ila kwa sasa changamoto hiyo imepata suluhu kupitia mradi wa maji.

Na Mindi Joseph.
Upatikanaji wa Maji safi na salama katika Mtaa wa Vikonje A Kata ya Mtumba Mkoani Dodoma umeimarika kwa saa 24.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Vikonje A Mkoani Dodoma Obed Majenda anasema hii ni kufuatia Wakala wa Nishati Vijijini(REA) kufikisha huduma ya umeme katika mradi wa Kisima cha Maji.

Sauti ya Bw.Obed Majenda.

Kwa upande wa wananchi nao wamepongeza Wakala wa Nishati Vijijini(REA) kwa kuwatatulia changamoto hiyo.

Sauti za wananchi.