Dodoma FM

Rais Samia kuzindua rasmi SGR Dodoma

30 July 2024, 7:46 pm

Picha ni mkuu wa mkoa wa Dodoma Mh. Rosemery Senyamule akiongea na vyombo vya habari .Picha na Fred Cheti.

Ikumbukwe kuwa tangu Treni ianze safari zake Kutoka Dar es Salaam kuja Dodoma zaidi ya wananchi 900 hadi 1000 wananufaika na usafiri huo. 

Na Fred Cheti.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani anatarajia kuzindua Rasmi Treni ya umeme (SGR) jijini Dodoma. 

Akizungumza na Vyombo vya habari Jijini Dodoma Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amesema RAIS Samia ataizindua Rasmi Agost 1mwaka huu eneo la Mkonze Jijini Dodoma ambapo wananchi wamejiandaa kutumia Reli kukuza fursa za kibiashara. 

Sauti ya Mh. Rosemery Senyamule.

Katika hatua nyingine akizungumza na waendesha bodaboda na Bajaji ambao watafanya kazi kwenye eneo Hilo, amewataka kuwa waaminifu, waadilifu na usafi wanapowasafirisha abiria jambo ambalo litasaidia kuutangaza Mkoa wa Dodoma na fursa zilizopo. 

Sauti ya Mh.Rosemery Senyamule.

Akizungumza kwa niaba ya maafsa usafirishaji (bodaboda) katibu Chacha Marwa amesema wanaishukuru Serikali kwa kuwajengea miundo mbinu ya kujipatia fedha na Kuahidi kutoa ushirikiano kwa Serikali kwa kufuata miiko ya kazi. 

Sauti ya Chacha Marwa.