Dodoma FM

Wananchi watakiwa kutoa ushirikiano polisi vitendo vya ukatili

24 July 2024, 4:40 pm

Picha ni waumini wa kanisa hilo wakiwa katika ibada ya kuwasimika viongozi.Picha na Yussuph Hassan.

Kanisa la Pentecostal Convent Faith lililopo Njedengwa Dodoma limesimika Viongozi mbalimbali wa Kanisa hilo ikiwemo Wachungaji zaidi ya watano na Wainjilisti.

Na Yussuph Hassan.
Wananchi Mkoani Dodoma wametakiwa kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi dhidi ya vitendo vya ukatili ikiwemo matukio ya Watoto kupotea, ukatili na ubakaji.

Wito huo umetolewa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Pentecostal Convent Faith Dodoma, Damas Silvesta katika ibada maalum ya kusimika Wachungaji zaidi ya watano na Wainjilisti.

Sauti ya Damas Silvesta .
Picha ni waumini wa kanisa hilo wakiwa katika ibada ya kuwasimika viongozi.Picha na Yussuph Hassan.

Ameongeza kuwa jamii haina budi kuendeleza maombi katika kukemea vitendo hivyo.

Sauti ya Damas Silvesta .

Kwa upande wao baadhi ya Viongozi waliyosimikwa katika ibada hiyo wameahidi kuitumikia vyema jamii na kanisa kwa ujumla.