Dodoma FM

Jamii zatakiwa kutumia taasisi za kitafiti kujifunza

17 July 2024, 2:38 pm

Picha ni Mbuzi wanao fugwa katika kituo cha utafiti wa mifugo Mpwapwa.Picha na Steven Noel.

lengo la ziara hiyo ni kutekeleza Sera ya Elimu ya mwaka 2023 na kuwaongezea watoto ari ya kujifunza masomo ya amali.

Na Steven Noel.
Jamii imeshauriwa kuzitumia taasisi za kitafiti katika kujifunza na kujiongezea uelewa wa mambo mbalimbali yahusuyo maendeleo na taaluma.

Rai hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Mpwapwa alipokuwa akiongea na walimu na wanafunzi 86 wa darasa la saba shule ya msingi Mpwapwa waliotembelea kituo hicho kwa ajili ya mafunzo.

Sauti ya mkurugenzi mtendaji wa tasisi ya utafiti wa mifugo Mpwapwa .

Happynes Kaungu ni Mkuu wa shule Mpwapwa shule ya Msingi wakati Amos Fundi Chuma ni mwalimu wa darasa. Wanasema lengo la ziara hiyo ni kutekeleza Sera ya Elimu ya mwaka 2023 na kuwaongezea watoto ari ya kujifunza masomo ya amali.

Sauti za walimu wa shule ya msingi Mpwapwa.