Dodoma FM

Wakazi wa Membe wapongeza ujenzi wa bwawa

4 June 2024, 5:55 pm

Mradi huo utaleta mabadiliko ya kiuchumi kwa wakazi wa Membe.Picha na NIRC

Ujenzi wa bwawa hilo limefikia asilimia 82 ambapo hatua inayoendelea ni ujenzi wa mifereji ya maji

Na Victor Chigwada.
Wakazi wa Kata ya Membe Wilaya ya Chamwino wameipongeza serikali kwa juhudi zinazoendelea katika ujenzi wa bwawa la kilimo cha Umwagiliaji.

Wakizungumza na Taswira ya Habari baadhi ya wananchi wameelezea mradi huo ambapo wamesema utaleta mabadiliko ya kiuchumi kwa wakazi wa Membe pamoja na wawekezaji wengine watakao jikita katika kilimo cha umwagiliaji

Kwa upande wake Mhandisi wa mradi huo kutoka Tume ya Taifa ya umwagiliaji Salehe Hamadi amesema kuwa ujenzi wa bwawa hilo limefikia asilimia 82 ambapo hatua inayoendelea ni ujenzi wa mifereji ya maji .

Sauti ya Salehe Hamadi

Mhandisi Hamadi amekiri uwepo changamoto katika tuta ambalo liliharibiwa na mvua .

Sauti ya Salehe Hamadi

Naye Diwani wa Kata ya Membe Bw.Simoni Macheho amewasihi wananchi wake kuwa tayari kuchanagamkia mradi huo ile waweze kukuza uzalishaji wa mazao .

Sauti ya Diwani wa Kata ya Membe