Dodoma FM

Klabu za maadili zaanzishwa kwa shule za msingi, sekondari Dodoma

17 May 2024, 12:25 pm

Wanafunzi wanafundishwa maadili yanayopaswa kuzingatiwa katika kutengeneza kizazi chenye uadilifu.

Lengo la klabu za maadili ni kuwajengea wanafunzi misingi bora ya maadili tangu wakiwa shuleni.

Na Mindi Joseph.
Zaidi ya klabu 200 za maadili kwa shule za sekondari na msingi zimeanzishwa mkoani Dodoma huku lengo ni kufikia shule zote kujenga ufahamu kwa watoto kuhusu maadili.

Wanafunzi wanafundishwa maadili yanayopaswa kuzingatiwa katika kutengeneza kizazi chenye uadilifu kwa siku zijazo.

Joshua Amoni ni afisa maadili kutoka Sekretarieti ya Maadili Kanda ya Kati Mkoa wa Dodoma anasema wanajenga msingi kwa watoto angali wadogo.

Sauti ya Bw. Joshua Amon

Kwa upande wake Lydia Mwakibete anasema wamekuwa wakifanya ufuatiliaji wa klabu za maadili mara kwa mara kwa watoto kuona zinafanya kazi kama ilivyokusudiwa.

Sauti ya Bi Lydia Mwakibete