Utupaji wa taka ngumu katika mifumo ya maji taka wachangia kuziba kwa mifumo
26 March 2024, 7:13 pm
Mhandishi Aron Joseph akiwa sambamba na wataalamu kutoka Mamlaka hiyo na Viongozi wa kata hiyo kufanya Ziara katika mtaa huo ambao unakabiliwa na changamoto ya kuziba kwa mifumo ya maji taka .
Na Seleman Kodima.
Utupaji taka ovyo katika mifumo ya maji taka katika mtaa wa kitenge ,Bahi road kata ya Majengo umetajwa kuwa ni kikwazo mojawapo kinachosababisha uwepo wa changamoto za mara kwa mara katika mfumo wa maji taka eneo hilo.
Hayo yamebainika baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa mazingira DUWASA Mhandishi Aron Joseph akiwa sambamba na wataalamu kutoka Mamlaka hiyo na Viongozi wa kata hiyo kufanya Ziara katika mtaa huo ambao unakabiliwa na changamoto ya kuziba kwa mifumo ya maji taka .
Akizungumza baada ya kutembelea maeneo yenye changamoto hiyo,Mhandisi Aron amewasihi wananchi wa mtaa huo kuzingatia matumizi sahihi ya mifumo ya maji taka na kuacha kutupa taka ngumu katika mifumo hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Mhandisi Benard Rugayi amesema licha ya DUWASA kuendelea kazi ya kuzibua chemba katika barabara inayojengwa katika mtaa huo bado wananchi wa mtaa huo wamekuwa ni sehemu ya changamoto .
Nae Diwani wa Kata ya Majengo Bi Shufaa Ibrahim amesema baada ya kubaini sababu za kuziba mara kwa mara kwa mifumo ya maji taka ndani ya mtaa huo watachukua hatua ya kuitisha mkutano wa mtaa ili kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya mifumo hiyo.
Pamoja na hayo Viongozi wa mtaa huo akiwamo mtendaji wa mtaa kitenge Bi zuwena Jabu na Mwenyekiti wa Ccm tawi la Bahirodi Sungura Mohamed wameshukurua hatua zilizochukuliwa na DUWASA kuhusu changamoto hiyo na wameahidi kutoa elimu kwa wananchi wao.