Dc kongwa akerwa na ubadhirifu wa fedha 6,394,000/=
18 April 2023, 3:39 pm
Katika taarifa iliyosomwa inaonyesha kiasi cha shilingi milioni 6,394,000 hazijathibitika matumizi yake
NA Bernadetha Mwakilabi, Kongwa
Mkuu wa wilaya ya Kongwa Mheshimiwa Remidius Mwema Emmanuel ameagiza ofisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU wilaya ya Kongwa kufanya uchunguzi juu ya ubadhilifu wa fedha uliofanywa na mwenyekiti wa kijiji cha Hogoro.
Agizo hilo limetolewa mapema baada ya taarifa ya mkaguzi wa ndani kuonesha kuwa kuna upotevu wa fedha za wananchi katika kijiji cha Hogoro uliofanywa na mwenyekiti wa kijiji hicho bwana Stephano Mgube
Pia Mwema amefafanua kuwa baada ya kubaini ukweli wa tuhuma hizo mtuhumiwa atafikishwa katika vyombo vya Sheria kwaajili ya kuwajibishwa.
Akisoma ripoti ya mkaguzi wa mahesabu kwa niaba ya mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kongwa mkaguzi wa ndani wa halmashauri ya Kongwa bi Jackline Kigwa amesema kiasi cha shilingi milioni 6,394,000 hazijathibitika matumizi yake.
Sambamba na hayo Mheshimiwa mwema amesema katika uongozi wake hatofumbia macho masuala ya ubadhilifu wa fedha Rushwa na ufisadi.