Migogoro baina ya viongozi Bolisa yazorotesha maendeleo
18 April 2023, 1:24 pm
Katibu wa jumuiya ya wazazi wa chama cha mapinduzi wilayani humo amekemea mwenendo wa migogoro hiyo kwani itawagharimu katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa.
Na Nizar Mafita.
Migogoro na maslahi binafsi ya viongozi na wananchi katika Kata ya Bolisa Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma imetajwa kuchochea ucheleweshwaji wa miradi ya maendeleo katika Kata hiyo
Mbunge huyo akiwa katika ziara ya siku moja ndani ya kata ya bolisa wilayani kondoa amebaini migogoro baina ya viongozi wa chama na kata huku wananchi wakitajwa kuchangia uwepo wa migogoro hiyo ikiwemo mvutano uliopo baina ya wananchi juu ya mtaa gani unapaswa kujengwa majengo ya shule.
Wakizungumza mbele ya mbunge huyo baadhi ya wananchi wa kata bolisa wamesema changamoto kubwa inaanzia kwa uongozi wa ngazi ya juu ndani ya kata.
Kwa upande wake diwani wakata hiyo Ramla Abeid amesema hana mgogoro wowote kati yake na wananchi wala mbunge.