Dodoma FM

Mikopo ya kausha damu yawatesa Ngh’ambaku

13 Aprili 2026, 11:46

Jamii bado inahitaji elimu ya kutosha juu ya mikopo  ili kufahamu madhara ya mikopo umiza.Picha na mtandao.

Mikopo umiza imekuwa ikipelekea athari nyingi kwa jamii ikiwemo familia zinazo jiingiza kwenye mikopo hiyo kukumbwa na madeni yasiyo kwisha.

Na Victor Chigwada

Wakazi wa Kata ya Ngh’ambaku Wilayani Chamwino wametakiwa kuachana na mikopo umiza maarufu kama kausha damu kwani imekuwa ikiathiri maisha yao.

Akiongea na Taswira ya habari Afisa maendeleo wa Kata ya Ngh’ambaku Bw.Richad Kisubi amesema jamii bado inahitaji elimu ya kutosha juu ya mikopo  ili kufahamu madhara ya mikopo umiza na kuchukua mikopo rafiki ikiwemo mkopo nafuu wa asilimia 10 unao tolewa na serikali.

Aidha amewataka wananchi kabla ya kuchukua mikopo hiyo ni vema kupitia Kwa makini masharti ya mtoa mkopo ili kuepuka upotevu wa mali na kufilisiwa baada ya kushindwa kurejesha mkopo huo.

Sauti ya Bw.Richad Kisubi.

Kisubi ameongeza kuwa mikopo umiza imekuwa ikipelekea athari nyingi kwa jamii ikiwemo familia zinazo jiingiza kwenye mikopo hiyo kukumbwa na madeni yasiyo kwisha na kupelekea ugumu wa maisha ulio kithiri.

Sauti ya Bw.Richad Kisubi.

Nao baadhi ya wananchi hususani kundi la akina mama ambalo ndilo limekuwa likiathirika zaidi na mikopo hiyo wameeleza ni kwanini wamekuwa wakiingia katika mikopo hiyo.

Sauti za wanawake