Dodoma FM

Viongozi wa umma watakiwa kuendelea kuzingatia maadili

9 April 2026, 17:06

Picha ni Katibu msaidizi sekretarieti ya maadili ya umma kanda ya Kati bi Jasmin Awadhi.Picha na Dodoma fm.

Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma ni taasisi iliyo chini ya ofisi ya rais kwa kusimamia maadili ya viongozi wa umma katika uwajibikaji wa shughuli mbalibali.

Na Jerome John.

Viongozi wa umma nchini wamekumbushwa kuendelea kuzingatia suala la maadili na kanuni au taratibu wanazopaswa kuzizingatia wakati wa kutekeleza majukumu yao.

Akizungumza na Taswira ya Habari, Katibu msaidizi sekretarieti ya maadili ya umma kanda ya Kati bi Jasmin Awadhi amesema kuwa suala la maadili lipo wazi kwa viongozi wa umma na kuwataka kufanya kazi kwa kuzingatia maslahi ya umma kwa uadilifu, uwazi,uaminifu na kuongoza kwa kuzingatia sheria za nchi.

Aidha amewakumbusha viongozi wa umma kufanyakazi kwa kuweka mipaka ili kuondoa mgongano wa maslahi kwa kutotumia rasirimali za umma kwa kujinufaisha wao wenyewe.

Sauti ya bi Jasmin Awadhi.

Katibu msaidizi huyo amewakumbusha wananchi kutoa taarifa sahihi juu ya viongozi wanao kiuka kanuni au taratibu ili uchunguzi uweze kufanywa na kama kuna ukweli hatua zichukuliwe.