Dodoma FM

Wanahabari watakiwa kuhabarisha umma majukumu ya sekretarieti ya maadili

2 April 2026, 17:10

Picha ni mkurugenzi wa mipango sekretarieti  ya maadili ya umma Omary Juma akiongea na waandishi wa habari.Picha na Bennard Filbert.

Semina hiyo imefanyika Dodoma na kupendekezwa kwa mipango kazi baina ya waandishi na sekereterieti hiyo kuona namna bora ya kuongeza juhudi za uhabarishaji jamii katika masuala ya maadili,uwajibika ,uzalendo,uwazi na uadilifu kwa viongozi wa umma na jamii kwa ujumla.

Na Jerome John.

Waandishi wa Habari kutoka mikoa ya kanda ya kati wametakiwa kutumia weledi wao kuhabarisha umma juu ya majukumu ya sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma.

Wito huo umetolewa na Bi.Jasmin Bakari katibu msaidizi wa sekretarieti  ya maadili ya umma kanda ya kati,wakati wa semina ya waandishi wa Habari juu ya majukumu ya sekretarieti hiyo.

Katibu msaidizi huyo amesema suala la maadili ya umma nila jamii nzima hivyo inawajibu wa kutekeleza jukumu hilo na kuhakikisha maadili mema sio tu kwa viongozi bali hata kwa jamii kutambua uwajibikaji na uwazi katikautendaji wa shughuli za umma.

Sauti

Aidha kwa upande wake mkurugenzi wa mipango Omary Juma amesisitiza juu ya ushirikiano baina ya waandishi na sekretarieti kwa kutoa taarifa pindi kiongozi wa umma anapokiuka maadili katika jamii.