Dodoma FM
Dodoma FM
27 March 2026, 17:43

Shule hiyo inakabiliwa pia na uhaba wa matundu ya vyoo hali inayo hatarisha usalama wa afya za wanafunzi na walimu.
Na Victor Chigwada.
Wakazi wa kijiji Cha Ndogowe wameiomba serikali kukarabati majengo ya shule ya msingi Ndogowe kwani ni chakavu sana pamoja na ukosefu wa matundu ya vyoo.
Wakiongea na Taswira ya habari wazazi hao wamesema wanahofia usalama wa watoto wao wawapo shuleni kwani majengo wanayo tumia kusoma ni chakavu sana.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Ndogowe Bw.Keneth Muhawi amekiri shule hiyo kukabiliwa na uchakavu wa majengo hali inayopelekea wanafunzi kusomea nje chini ya mti.
Bw. Muhawi amesema licha ya uchakavu wa miundombinu shuleni hapo pia shule hiyo inakabiliwa pia na uhaba wa matundu ya vyoo hali inayo hatarisha usalama wa afya za wanafunzi na walimu.