Dodoma FM

Vijana Dodoma kunufaika na fursa za kiuchumi

26 March 2026, 17:52

Picha ni baadhi ya viongozi na vijana walio hudhuria kikao hicho.Picha na Dodoma cc news.

Vijana hao watumike katika mikutano na makongamano kuonesha jamii kuwa mabadiliko ya tabia za kiuchumi yanawezekana” alisema Dkt. Kazungu.

Na Mariam Kasawa.

Vijana waliopatiwa mafunzo na kujengewa uwezo kupitia Mradi wa AHADI wanatarajiwa kunufaika ipasavyo na fursa za kiuchumi zilizopo, huku ufuatiliaji wa karibu ukihimizwa ili kuhakikisha ujuzi walioupata unazaa matokeo chanya katika kujiajiri na kukuza vipato vyao.

Hayo aliyasema Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Dkt. Khatibu Kazungu wakati akifunga kikao cha kujadili ufuatiliaji na utekelezaji wa Mradi wa AHADI unaofanywa na Shirika la TAHEA kilichofanyika mkoani Dodoma.

Alieleza kuwa serikali imewekeza rasilimali nyingi katika kuwawezesha vijana kupitia mafunzo ya ujasiriamali, stadi za maisha na ujuzi wa kujiajiri. Hivyo, ni wajibu wa maafisa maendeleo ya jamii na maafisa vijana husika kuhakikisha uwekezaji huo unaleta matokeo chanya kwa vijana na jamii kwa ujumla.

Picha ni baadhi ya viongozi na vijana walio hudhuria kikao hicho.Picha na Dodoma cc news.

Alisisitiza kuwa viongozi wa Mradi wa AHADI kwa kushirikiana na maafisa maendeleo ya jamii na maafisa vijana kuhakikisha vijana waliofanikiwa wanakuwa mabalozi kwa vijana wengine. “Kupitia vijana waliofanikiwa kwa kuajiriwa au kujiajiri wanapaswa kuwa mabalozi kwa kutoa hamasa kwa vijana wengine.

Nae, Mratibu wa Mradi wa AHADI ngazi ya jiji, Lorner Mziray alisema kuwa kupitia mradi huo vijana wengi wamefikiwa kwa kuwezeshwa kipato.

Kwa upande wake mnufaika wa Mradi wa AHADI, Ally Ally alieleza kuwa mradi umetoa mabadiliko makubwa kwa vijana wengi. “Kupitia mradi huu vijana wengi tumeweza kuajiriwa na wengine kujiajiri wenyewe kwasababu tulipewa mafunzo lakini baada ya hapo ndipo tukaajiriwa hadi sasa.