Dodoma FM
Dodoma FM
20 March 2026, 17:12

Muhawi ameongeza kuwa wengi wao wamekuwa na wasiwasi wa kutokuaminiana kwenye vikundi .
Na Victor Chigwada.
Mwitikio mdogo wa vijana katika kuanzisha vikundi katika kijiji cha Ndogowe wilayani Chamwino umepelekea vijana kushindwa kunufaika na mikopo ya asilimia kumi inayo tolewa na halmashauri zote hapa nchinni kwa makundi ya vijana , wanawake na watu wenye ulemavu.
Akiongea na taswira ya habari Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bw.Keneth Muhawi amesema licha ya elimu kutolewa na Afisa maendeleo wa kata hiyo pamoja na hamasa mbalimbali lakini bado vijana hao hawana muamko wowote wa kuanzisha vikundi ili kunufaika na mikopo hiyo.
Taswira ya habari imemtafuta Afisa maendeleo wa Kata ya Ngh’ambaku Bw.Richadi Kasubi amekiri kuwa hadi sasa licha ya juhudi walizo fanya hawajafanikiwa kupata hata kikundi kimija cha vijana kutoka Ndogowe hivyo wanaendelea kutoa elimu kwa vijana hao ili kuwaongezea uelewa.
Aidha Kasubi ameongeza kuwa tayari upo mkakati wa kutoa semina Kwa vijana wote wa vitongoji vya kijiji hicho ili kuwapa hamasa na kuwaongezea uelewa wa mikopo ya asilimia 10 na faida ya vikundi.
Nao baadhi ya wakazi wa Kijiji hicho wamesema kuwa ni vema vijana kupokea elimu zinazo andaliwa Kwa Njia ya semina na Afisa maendeleo Kata Ili kunufaika na mikopo ya Serikali na mashirika mbalimbali.