Dodoma FM

Baadhi ya vijana Ndogowe watelekeza mashamba yao

19/03/2026, 16:53

Picha ni Shamba la pamoja la BBT Chinangali.Picha na Wizara ya kilimo.

Hayo yanajiri baada ya vijana wa mradi wa Jenga kesho iliyo bora (BBT)Kijiji Cha Ndogowe kuonekana kushindwa kuendelea na palizi katika mashamba Yao yaliyopo katika mpango huo .

Na Victor Chigwada.

Wanufaika wa mradi wa Jenga kesho iliyo bora BBT wametakiwa kujituma Kwa juhudi Ili kuona manufaa na maono ya Serikali ya kumkwamua kijana katika wimbi la ukosefu wa ajira kupitia kilimo.

Hayo yanajiri baada ya vijana wa mradi wa Jenga kesho iliyo bora (BBT)Kijiji Cha Ndogowe kuonekana kushindwa kuendelea na palizi katika mashamba Yao yaliyopo katika mpango huo .

Mwenyekiti wa Kijiji Cha Ndogowe Bw.Keneth Muhawi amesema vijana wengi wameshindwa kuendeleza shughuli za kilimo kutokana na kutegemea nguvu ya Serikali .

Sauti ya Bw.Keneth Muhawi .

Aidha ameongeza kuwa kutokana na baadhi ya vijana hao kushindwa kupalilia mashamba yao  hakuna matarajio makubwa ya kuvuna kwani mimea iliyopo katika mashamba hayo imefunikwa na majani marefu haiwezi kuleta mazao mazuri.

Sauti ya Bw.Keneth Muhawi .

Nao baadhi ya vijana walio endelea na kilimo Kwa juhudi zao wamewasihi vijana wenzao kuto kukata tamaa na kusimamia uwekezaji wa Serikali Kwa nguvu na kujiletea tija wao wenyewe.

Sauti za baadhi ya vijana.