Dodoma FM

Wananchi Chanh’umba walalamika baadhi ya mabomba kutotoa maji

18/03/2026, 17:19

Baadhi ya wananchi wameitupia lawama RUWASA kwa kushindwa kuendeleza mradi huo wa maji.Picha na Mtandao.

Mwenyekiti wa vitongoji hivyo Bw Amosi Lusiji amekiri zoezi la usambazaji miundombinu ya maji umekamilika Kwa asilimia kubwa katika vitongoji.

Na Victor Chigwada.

Wakazi wa vitongoji vya Arusha, Ilolo na kawawa Kijiji Cha Chanh’umba Wilayani Chamwino wameomba kufanyiwa ukarabati wa mabomba ya  maji ambayo Kwa Sasa hayatoi maji.

Wamesema licha ya  Serikali Kwa kushirikiana na shirika la water mission Kwa kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji katika vingoji hivyo na kusogeza huduma ya maji karibu lakini kumekuwa na tatizo la baadhi ya miundombinu ya mabomba kushindwa kutoa maji.

Sauti za wananchi.

Aidha wameiomba Serikali kuendelea kuongeza miradi ya maji katika maeneo mengine ya vitongoji vyao sanjari na eneo la zahanati yao

Sauti za wananchi.

Mwenyekiti wa vitongoji hivyo Bw Amosi Lusiji amekiri zoezi la usambazaji miundombinu ya maji umekamilika Kwa asilimia kubwa katika vitongoji.

Changamoto imekuwa Kwa wasimamizi wa maji vijijini RUWASA ambao wameonekana kushindwa kuendesha mradi huo Hali iliyo pelekea shirika la water mission kurejea na kuendelea na ukarabati wa mradi wao walio uanzisha.

Sauti ya Bw Amosi Lusiji .