Dodoma FM

Teknolojia yatajwa kuongeza ajira kwa vijana

17/03/2026, 17:58

Ukuaji wa teknolojia umeleta uwepo wa mitandao ya kijamii ambayo imerahisisha kutangaza biashara mbalimbali tofauti na zamani.Picha na Mtandao.

Kutokana na kukua kwa teknolojia nchini serikali imekuwa ikishauri vijana kuhakikisha wanatumia nafasi hiyo kujikwamua kiuchumi ikiwemo kujitangaza pamoja na kutengeneza maudhui yanayo endana na mila na tamaduni za kitanzania.

Na Mwanahamis Badi.

Ukuaji  wa teknolojia umetajwa  kutengeneza fursa mpya za ajira kwa vijana nchini na kuachana na dhana ya kuajiriwa.

Baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii Dodoma wamezungumza na Dodoma fm ambapo wamesema ukuaji wa teknolojia umepelekea uwepo wa mitandao ya kijamii ambayo imerahisisha kutangaza biashara mbalimbali tofauti na zamani.

Aidha wamesema   mitandao ya kijamii imeajiri vijana wengi ikiwemo kwenye sekta ya sanaa ambapo baadhi yao wamekuwa wakitumia fursa hiyo kutengeneza maudhui ambayo yana waletea fedha.

s