Dodoma FM

Mvua yasomba mashamba kwa Mshango Mpwapwa

16/03/2026, 18:11

Picha ni moja ya shamba ambalo limejaa maji kutkana na mvua za masika zinazo endelea kunyesha.Picha na Steven Noel.

Amesema taarifa hiyo tayari imeandaliwa na itawasilishwa katika ofisi za ngazi ya wilaya kwa hatua zaidi.

Na Stephen Noel, Mpwapwa

Mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini zimeendelea kusababisha madhara kwa wananchi, ikiwemo kusombwa kwa mashamba ya wakulima katika Kitongoji cha Kwa Mshango, wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.

Wakizungumza na Taswira ya  Habari, baadhi ya wananchi wa kitongoji hicho wamesema uharibifu wa mazingira unaoendelea katika maeneo ya milima ya Mdyanga, Kiboliani na Nguji umechangia maji kujaa kwa kasi na kusomba mashamba yao, hali iliyosababisha hasara kubwa kwa wakulima.

Kwa upande wake, Afisa Kilimo wa Kata ya Vighawe, Bi. Bhoke Magere, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa ofisi ya kata imefanya tathmini ya awali ili kubaini kiwango cha hasara iliyotokea.

Aidha, wananchi wa eneo hilo wameiomba serikali kuwasaidia mbegu ili waweze kuanza upya shughuli zao za kilimo baada ya mashamba yao kuharibiwa na maji ya mvua.

Sauti ya Steven Noel