Dodoma FM
Dodoma FM
16/03/2026, 17:58

Barabara hiyo ambayo inaunganisha Mkoa wa tanga na Manyara inaendelea kufanyiwa ukarabati.
Na Kitana Hamis.
MVUA kubwa zinazoendelea kunyesha Wilayani Kiteto, Mkoani Manyara zimesababisha kukatika kwa mawasiliano ya barabara ya na kupelekea adha kubwa kwa watumiaji wa barabara hiyo.
Wakiongea na Taswira ya habari wananchi wa eneo hilo wameiomba serikali kukarabati barabara hiyo kwani inapelekea kukwama kwa usafiri.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kiteto Mh. Remidius Mwema amesema barabara hiyo ambayo inaunganisha Mkoa wa tanga na Manyara inaendelea kufanyiwa ukarabati na ipo kwenye mpango wa serikali tayari.