Dodoma FM
Dodoma FM
16/03/2026, 17:47

VIJIJI vitakavyo nufaika na mpango huo ni Kijiji cha Mzase,Godegode,Mgoma Kisisi na Kitati.vijiji vingine Lukole Kingiti na Kidenge .
Na Steven Noel.
JUMLA ya vijiji nane vya halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa mkoa wa Dodoma vinatarajia kunufaika mpango wa matumizi bora ya Ardhi ambao inatekelezwa na tume ya taifa ya mipango ya matumizi ya Ardhi .
Akiongea Afisa kutoka tume ya Taifa ya mipango ya taifa ya matumizi ya Ardhi bwana Amos Mluga amesema mpango huo utatekelezwa Katika vijiji nane na vitasaidia kupunguza migovoro ya wakulima na wafugaji lakini pia kupunguza migovoro ya mipaka kati ya vijiji na vijiji .
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa bi Mwanahamis Aly amesema mpango huo utakuwa na tija Kwa halmashauri hiyo ikiwa na kukuza thamani ya Ardhi lakini pia itakuwa mwarobaini ya migogoro ya mipaka wakati Kaimu Afisa Ardhi wa wilaya hiyo Bi Jeny Mbelwa amesema itawasaidia kuwajengea uwezo Jamii Katika matumizi bora ya rasilimali Ardhi na kusaidia kutunza mazingira.
Naye kaimu mwenyekiti wa halmashauri hiyo na Diwani kata ya Berege bwana Baraka Habari amesema
Baadhi ya Wananchi ambao ni wanufaika wa mpango huo wakielezea manufaa ya mpango huo wamesema.