Dodoma FM
Dodoma FM
23/02/2026, 15:47

Mwenyekiti wa mtaa wa Bwawani ameeleza hatua ambazo zinaendelea hadi sasa kuhusu ubomoaji huo.
Na Farashuu Abdallah.
Ikiwa miezi kadhaa imepita tangu wananchi wa Mtaa wa Bwawani kata ya Mkonze jijini Dodoma kutoa malalamiko yao kuhusu uamuzi uliochukuliwa na ofisi ya Mkurugenzi wa kubomoa nyumba zao bila taarifa yoyote, mwenyekiti wa mtaa huo ametolea ufafanuzi suala hilo.
Akizungumza na Dodoma FM Mwenyekiti wa mtaa wa Bwawani Bw. Sospeter Abeli amesema kuwa kinachosubiriwa hivi sasa ni mazungumzo baina ya viongozi wa mtaa na ofisi ya mkurugenzi.
Aidha Mwenyekiti huyo amemaliza kwa kuwasihi wananchi kuendelea kuwa na subira huku mchakato wa kutatua changamoto hiyo ukiwa unaendelea.