Dodoma FM

Ulinzi waendelea kuimarishwa Mtumba na viunga vyake

20 February 2026, 5:58 pm

OCD  Chau amesema kuwa IPO mipango ya kuhakikisha wanakomesha tabia hizo zinazo ibuka.Picha na Full shangwe.

Aidha ameongeza kuwa Hali hiyo inaweza kuchangia na kusahaulika Kwa majukumu ya kiulinzi na usalama na kupelekea kurejea Kwa matukio hayo.

Na Victor Chigwada.

Mkuu wa kituo Cha polisi Wilaya ya Mtumba kamanda OCD Issa Chau ameeleza  Hali ya ulinzi na usalama katika Wilaya hiyo hususani Kata ya Ihumwa ambayo imekuwa na matukio ya wizi katika maduka na mifugo

Chau ameeleza kuwa miongoni mwa maeneo ambayo walifanikiwa kudhibiti wimbi la uhalifu ilikuwa ni ihumwa tofauti na Sasa inavyo ripotiwa

Aidha OCD  Chau amesema kuwa IPO mipango ya kuhakikisha wanakomesha tabia hizo zinazo ibuka kwani wananchi wamekuwa na utayari wa kuunga mkono jitihada za ulinzi na usalama

Sauti ya OCD  Chau.

Chau amesema kuwa wako tayari kufanya oparesheni za kutatua changamoto ya udozi na wizi wa Mali za wananchi Kwa kufuatilia hata uaminifu wa baadhi ya watumishi ikiwa ni pamoja na migambo wa doria

Sauti ya OCD  Chau.