Dodoma FM

Zao la zabibu kuanza kutangazwa nchini Burundi

17/02/2026, 16:47

Balozi wa Tanzania nchini Burundi Mhe. Gelasius G. Byakanwa akiwa na mkuu wa mkoa wa Dodoma Mh.Rosemery Senyamule.Picha na Mkoa wa Dodoma.

Kuanza kutangazwa kwa zao la zabibu nchini Burundi kumefurahisha baadhi ya wachakataji na wazalishaji wa mvinyo, na kusema kuwa watajitahidi kuzalisha bidhaa zenye ubora na viwango vya kimataifa .

Na Mariam Kasawa.

Balozi wa Tanzania nchini Burundi Mhe. Gelasius G. Byakanwa, amefanya kikao Februari 16,2026 na wazalishaji na wachakataji wa zao la Zabibu wanaozalisha Mvinyo (Wine) Mkoa wa Dodoma akilenga kutangaza bidhaa hiyo nchini Burundi ambayo ni ya kipekee kuzalishwa nchini Tanzania katika Mkoa wa Dodoma.

Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jengo la Mkapa Jijini hapa ambapo Mhe. Balozi Byakanwa amesema anaandaa maonesho ya Mvinyo unaozalishwa Dodoma nchini Burundi mwezi Mei, 2026, ambapo wachakataji hao watapata fursa ya kutangaza soko lao nchini humo.

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, amepongeza jitihada za Balozi huyo kutangaza soko la Mvinyo nchini Burundi na kusema kuwa hatua hiyo itakwenda kumaliza kabisa changamoto ya upatikanaji wa soko la zabibu hususan kinywaji adhimu cha Mvinyo kwani Dodoma imekua na uzalishaji mkubwa lakini soko ndio limekua si la uhakika.

Sauti ya Mhe. Gelasius G. Byakanwa, na Senyamule.