Dodoma FM
Dodoma FM
5 February 2026, 4:47 pm

Uzinduzi wa mradi wa nishati safi ya kupikia katika shule ya sekondari Bunge Wasichana Mkoani Dodoma umeenda sambamba na uzinduzi wa klabu ya kwanza ya masomo ya nishati safi ya kupikia kwa ajili ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia na kubuni tenkolojia za kupikia zinazolinda afya.
Na Anwary Shaban.
Imeelezwa kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa kwenye matumizi ya nishati safi ya kupikia kutoka asilimia 6.9 kwa mwaka 2021 hadi 25.2 kwa mwaka 2025.
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Nishati Salome makamba katika uzinduzi wa mradi wa nishati safi ya kupikia katika shule ya sekondari Bunge Wasichana Mkoani Dodoma.
Aidha amezitaka sekta binafsi kuchangamkia fursa ya matumizi ya nishati safi katika maeneo yenye uhitaji.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wizara ya Nishati James Mataragio amesema uzinduzi wa mradi wa nishati safi ya kupikia katika shule ya sekondari Bunge Wasichana ni ishara ya serikali katika kueneza mabadiliko ya matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Naye Kaimu Mkuu wa Shule Richard Misana kupitia taarifa ya shule amepongeza mradi huo kwani umepunguza matumizi makubwa ya fedha waliyokuwa wakinunua nishati nyengine ikiwemo kuni na mkaa hapo awali.