Dodoma FM
Dodoma FM
30 January 2026, 5:32 pm

Airtel Tanzania inaendelea kuipa kipaumbele upanuzi wa mtandao kama sehemu ya dhamira yake ya kukuza ujumuishi wa kidijitali, kuhakikisha wananchi wote nchini wanapata huduma za simu na intaneti zenye uhakika, gharama nafuu, na ubora wa juu.
Na Bennard Komba
Kampuni ya mawasiliano nchini AIRTEL TANZANIA imeendelea kujiweka karibu zaidi na wananchi baada ya kufanikiwa kuzindua minara mitano mipya katika maeneo mbalimbali nchini.
Minara hiyo mipya imezinduliwa katika eneo la kilindi Tanga, Mbalamaziwa – Njombe, Ruanda – Songea, Miombo – Sumbawanga, na Buhongwa – Mwanza, hatua inayolenga kuimarisha upatikanaji wa mtandao na kuboresha huduma za simu na intaneti kwa wananchi wanaoishi katika maeneo hayo
Mkazi wa Miombo, Sumbawanga ambaye ameshuhudia uzinduzi huo ameshukuru kampuni ya airtel Tanzania kwa kuzindua minara mipya huku akisema.
Douglas Mwingira ni Diwani wa Kata ya Ruanda mkoani Ruvuma ameishukuru Airtel kwa kuwekeza katika eneo hilo, akibainisha kuwa mnara huo utakuwa kichocheo cha maendeleo ya haraka.
Bi. Lydia Kalimunda ni Meneja wa Tawi la Airtel Tanga amesema mnara huo mpya utakuwa na mchango mkubwa katika kuwaunganisha wakazi na fursa zilizo nje ya maeneo yao ya karibu
Naye Bw. Malaki Mchala ni Meneja wa Kanda wa Airtel Mwanza wakati Tukio la uzinduzi likifanyika Buhongwa ameleza athari chanya za mnara huo katika maisha ya kila siku na maendeleo ya wananchi