Dodoma FM

Serikali yasisitiza wajibu wa familia na jamii katika kuwahudumia wazee

28 January 2026, 2:10 pm

Picha ni Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi, katika ufunguzi wa Bunge la 13, jijini Dodoma. Picha na Mariam Matundu.

Hata hivyo, amebainisha kuwa Serikali itaendelea kuhamasisha maadili ya uwajibikaji wa kifamilia na kuimarisha mifumo ya kijamii inayosaidia ustawi wa wazee nchini.

Na Mariam Matundu.

Serikali imesema haina haja ya kuweka sharti la kisheria linalowalazimisha watoto kuwahudumia wazazi wao wasiojiweza, ikieleza kuwa suala hilo tayari linashughulikiwa kupitia misingi ya kifamilia na kijamii.

Kauli hiyo imetolewa bungeni na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa kinondoni Mhe. Tarimba Gulam Abbas lililohoji “Je Serikali haioni haja ya kuweka sharti la kisheria la watoto wakubwa kutunza  wazazi wao wasiojiweza”?

Picha ni Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi, katika ufunguzi wa Bunge la 13, jijini Dodoma. Picha na Mariam Matundu.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Mahundi amesema Serikali inatambua umuhimu wa familia na jamii katika kuchukua jukumu la kulea na kuwahudumia wazee, akisisitiza kuwa huo ni msingi wa mila na desturi za watanzania.

Ameongeza kuwa serikali imeendelea kuimarisha huduma na matunzo kwa wazee kupitia utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Wazee ya mwaka 2003, Toleo la mwaka 2024, ambayo inasisitiza wajibu wa familia na jamii katika kuwahudumia wazee wao.

Sauti ya Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi.