Dodoma FM
Dodoma FM
14 January 2026, 3:10 pm

Picha ni wageni kutoka nchini Malawi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma. Picha na Dodoma rrh.
Ujio wa ugeni huu unalenga kuimarisha ushirikiano wa kiafya kati ya Malawi na Tanzania, pamoja na kuchochea ubadilishanaji wa uzoefu miongoni mwa wataalamu wa afya.
Na Mariam Kasawa.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Afya Januari 13, 2026, imepokea ugeni kutoka nchini Malawi.
Ugeni huo, ukiongozwa na Waziri wa Afya wa Malawi, Mhe. Madalitso Baloyi, umetembelea Hospitali ya Rufaa ya Dodoma kwa lengo la kujifunza na kujionea utekelezaji wa mfumo wa usafiri wa dharura kwa mama wajawazito, akina mama waliojifungua hadi siku 42, pamoja na watoto wachanga wenye umri wa siku 0–28 (M-MAMA).
Aidha, ugeni huo ulikutana na viongozi wa sekta ya afya pamoja na wadau mbalimbali ili kubadilishana uzoefu na kujifunza mbinu bora za utoaji wa huduma za afya.
Katika ziara hiyo, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Thomas Rutachunzigwa, alishiriki kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.