Dodoma FM

Njaa yaanza kuwa tishio kwa wakazi wa Ndogowe

11 September 2025, 4:18 pm

Baadhi ya Wakazi hao wamesema kuwa kipindi hichi kimekuwa kigumu kwao kwani hawana chakula Cha kujitosheleza katika familia zao.Picha na Dodoma fm.

Wameongeza kuwa hali hiyo imewalazimu wanaume kuhama nyumbani na kwenda kutafuta fursa kwa ajili ya kukidhi uchumi wa familia.

Na Victor Chigwada.
Imeelezwa kuwa hali ya uhaba wa mvua katika msimu uliopita mwaka 2024/2025 imeaanza kuwaathiri wananchi wa kijiji cha Ndogowe kwani wanakabiliwa na changamoto ya chakula.

Baadhi ya Wakazi hao wamesema kuwa kipindi hichi kimekuwa kigumu kwao kwani hawana chakula Cha kujitosheleza katika familia zao.

Wameongeza kuwa hali hiyo imewalazimu wanaume kuhama nyumbani na kwenda kutafuta fursa kwa ajili ya kukidhi uchumi wa familia.

Sauti za wananchi.

Kenneth Muhawi mwenyekiti wa kijiji cha Ndogowe amekiri wakazi wake kuwa na changamoto ya kukosa chakula baada ya kumaliza kile walichopata katika msimu uliopita.

Muhawi ameongeza kuwa kwasasa baadhi ya familia zimebaki na wanawake kwani baadhi ya wanaume wamelazimika kwenda kutafuta vibarua maeneo ya nje na Kijiji Chao Ili kukidhi chakula katika familia zao.

Sauti ya Kenneth Muhawi.