Ukosefu wa taarifa na unyanyapaa vyatajwa makabiliano afya ya akili
28 January 2025, 6:31 pm
Lengo ni kuhakikisha Mapato yatakayopatikana yanachangia upatikanaji wa huduma hiyo.
Na Seleman Kodima.
Ukosefu wa taarifa sahihi ,unyanyapaa zimetajwa kuwa sababu zinazopeleka jamii kutojitokeza kushiriki afua za kukabiliana na magonywa ya changamoto za afya ya akili.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Hospitali taifa ya Mirembe Dkt Paul liwala wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hospitali hiyo kuandaa mbio kwa ajili ya kuchangia huduma ya afya ya akili kwa watoto.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa taasisi ya Vanessa Amada foundation Vanessa amesema lengo la kushirikiana na hospitali ya mirembe katika uandaji wa mbio hizo ni kuhakikisha Mapato yatakayopatikana yanachangia upatikanaji wa huduma hiyo.