Dodoma FM

Watu wenye Ualbino waomba kipaumbele mikopo ya 2%

22 November 2024, 12:08 pm

Picha ni Mathias jeremia kijana mwenye ualbino akiongea na Dodoma Tv.Picha na Steven Noel.

Mikopo hiyo itawasaidia kazi Katika mazingira rafiki na kujikinga  na ugonjwa saratani ya ngozi .Picha na Steven Noel.

Na Steven Noel.

Watu wenye ualbino wilayani ya Mpwapwa wameiomba halmashauri ya wilaya hiyo kuwapa kipaumbele Katika mikopo ya asilimia 2  ili wafanye kazi Katika mazingira rafiki na kujikinga  na ugonjwa saratani ya ngozi .

Hayo yamebainishwa na  mwenyekiti watu wenye Ualbino wilaya ya Mpwapwa Alpha Sweda katika  zoezi la uchunguzi wa ugonjwa wa saratani ya ngozi  na uwagawaji wa vifaa saidizi .

Sauti ya Bw. Alpha Sweda mwenyekiti wa watu wenye Ualbino Mpwapwa.

Mathias Jeremia ni  kijana mwenye ualbino anasema kutokana na ngozi za kushindwa kumili jua hivyo hushindwa kujishughulisha na shughuli za kilimo ambazo ndio shughuli za Wananchi wengi waishio vijijini na kusababisha kuishi maisha ya umaskini .

Sauti ya kijana Mathias Jeremiah
Picha ni baadhi ya misaada ambayo ilitolewa kwa watu wenye ualbino wilayani Mpwapwa.Picha na Steven Noel.

Kwa upande wake mratibu wa Afya kutoka shirika lisilo la kiserikali Innocent Mandu amesema wameamua kufanya uchuguz huo Kwa lengo  kupunguza  tatizo la saratani ya ngozi Kwa watu wenye ualbino.

Sauti ya Bw. Innocent Mandu.