TCRA yadhibiti utapeli mtandao
8 November 2024, 7:14 pm
Na Anwary Shabani
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA kanda ya kati imedhibiti uhalifu wa mitandao kwa kiwango kikubwa kupitia Kampeni ya Ni Rahisi Sana.
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA kanda ya kati Mhandisi Asajile John amesema kuwa kampeni hii inayosisitiza matumizi ya mtandao yanayozingatia usalama ili kuepusha matukio ya utapeli na udukuzi.
Aidha kwa wananchi wanaeleza jinsi walivyoelimika na kuepuka utapeli wa mtandao pamoja na athari zinazoweza kujitokeza endapo namba ya nida ikitumika kusajili laini zaidi ya moja.
TCRA inaendelea na Kampeni ya “Ni Rahisi Sana” inayosisitiza matumizi ya mtandao yanayozingatia usalama ili kuepusha matukio ya utapeli na udukuzi.