Dodoma FM
Hospitali ya Rufaa Dodoma yajipanga kupambana na utapiamlo
8 November 2024, 7:15 pm
Na Mindi Joseph
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma General imejipanga kupunguza adha inayoikabili jamii katika masuala ya Afya, kwa kuendelea kutoa Matibabu lishe kwa Watoto wenye utapiamlo mkali.
Hii inayojumuisha chakula dawa na kuwaandalia sehemu ya michezo kwa ajili ya uchangamshi.
Hayo yamebainishwa Afisa lishe Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma General Irene Cornelio.
Bi. Nusrat Swaibu ambaye ni afisa Lishe Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma anabainisha namna wanavyowaelimisha wazazi kuhusu mpangilio wa vyakula vya lishe kwa watoto.