Wananchi wataharuki tukio la mtu kujinyonga Dodoma
17 October 2024, 8:01 pm
Na Nazael Mkude.
Wakazi wa Mtaa wa Mathias Kata ya Miyuji Mkoani Dodoma wamepatwa na taharuki baada ya tukio la mtu mmoja kujingonga katika mtaa huo .
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Balaozi Shina Namba 5 wa Mtaa wa Mathias Bwn. Said Ali Madeni anasema kuwa marehemu alikuwa ni jirani yake ambaye alikuwa ni fundi ujenzi.
Bwn. Sulemani Zebedayo Mazego Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Mathias Kata ya Miyuji anaelezea jinsi alivyopata taarifa na hatua walizozichukua.
Wakiwa katika hali ya taharuki, baadhi ya wakazi wa mtaa huo ambao wanamfahamu marehem wamesilitishwa kutokea kwa tukio hilo.
Wakati huo Jeshi la Polisi limechukua nafasi hiyo kuwaasa wananchi kuwa wazi kwa wenza wao endapo watakuwa wanakabiliwa na changamoto binafsi zinazopelekea msongo wa mawazo . Tukio hilo limetokea oktoba 16, 2024 ambapo marehemu alifahamika kwa jina la Stanslaus Samira Osebio mwenyeji wa Iringa.