Dodoma FM

Wanafunzi chachu ya mabadiliko katika jamii

11 October 2024, 7:25 pm

Wanafunzi zaidi ya 900 kutoka shule 10 za sekondari Mkoani Dodoma wameshiriki Mdahalo wa kuwajengea uwezo wa kupambana na Rushwa,matumizi ya dawa za Kulevya na kijikinga na Maambukizi ya VVU.

Mdahalo huo umeandaliwa na Takukuru Mkoa kwa  kushirikiana na Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania,Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora unalenga kujenga jamii isiyo na rushwa.

Akizungumza na wanafunzi Leo Jijini Dodoma Afisa Uchunguzi Kiongozi na kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Dodoma Zacharia Mwandumbya anasema wanafunzi wa Sekondari wakipata elimu hii itakuwa chachu ya kufanya mabadiliko katika Jamii.

Afisa Uchunguzi Kiongozi na kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Dodoma Zacharia Mwandumbya
Suaati ya Bwn. Zacharia Mwandumbya

Kwa upande wa wanafunzi walioshiriki mdahalo huo wameahidi kusimama imara dhidi ya mapambano ya rushwa dawa za kulevya na kujikinga na maambukizi ya Vvu.

Pichani mwanafunzi akieleza umuhimu wa elimu waliyopata kupamabana na rushwa
Sauti za wanafunzi
Pichani mwanafunzi akieleza jinsi alivyopokea elimu ya kupambana na rushwa

Midahalo ya wanafunzi na wanavyuo kuhusu Rushwa mmomonyoko wa Maadali, kupinga matumizi ya dawa za kulevya, kuzuia maambukizi ya VVU na kuhamasisha utawala bora ni endelevu ili Kujenga uadilifu na jamii isiyo na rushwa.