Dodoma FM

DUWASA waaswa  matumizi ya kauli kwa mteja

7 October 2024, 6:59 pm

Na Fred Cheti                                                   

Watendaji wa mamlaka ya maji safi DUWASA wameaswa  kutumia kauli njema katika kuwahudumia wananchi kikamilifu ili kupunguza malalamiko .

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa mazingira Dodoma (DUWASA) Mha. Aron Joseph amesema hayo leo wakati wa uzinduzi wa wiki huduma kwa wateja iliyofayika katika ofisi za Malamka hiyo.

Uzinduzi huo umekwenda sambamba na zoezi la utoaji wa misaada mbalimbali katika hospitali ya St. Gemma ambao ni miongoni mwa wateja wakubwa wa mamlaka hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa mazingira Dodoma (DUWASA) Mha. Aron Joseph
Sauti ya Mha. Aron Joseph

Aidha Kwa Bi. Winifirda Kulanga Mtendaji DUWASA ametoa rai kwa wateja kulipa  ankara za maji kwa wakati ili kuwezesha mamlaka hiyo kujiendesha,

Bi. Winifirda Kulanga Mtendaji DUWASA
Sauti ya Bi. Winifirda Kulanga

Taasisi mbalimbali nchini leo zimezindua rasmi wiki ya huduma kwa wateja kwa lengo la kutoa elimu pamoja na kuhudumia wananchi.

Pichani Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa mazingira Dodoma (DUWASA) Mha. Aron Joseph akikata utepe kuashiria uzinduzi wa wiki ya huduma kwa mteja