Dodoma FM

Kongwa mfano wa kuigwa utekelezaji  miradi ya maendeleo

7 October 2024, 7:01 pm

Na Fred Cheti                                         

Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma imekuwa kinara katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule, amebainisha hayo katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo Wilayani Kongwa wakati akiambatana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe. Hamad Y. Masauni (MB) ambapo moja ya mradi wa ujenzi wa maabara ulikaguliwa mwishoni mwa wiki jana.  

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule
Sauti ya Mhe. Rosemary S. Senyamule,

Aidha Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe. Hamad Y. Masauni (MB), amesema kuwa ujenzi wa maabara hiyo itachagiza kasi kwa  wanafunzi kusoma masomo ya sayansi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe. Hamad Y. Masauni (MB)
Sauti ya Mhe. Hamad Y. Masauni (MB)

Waziri wa Mambo ya Ndani anaendelea na ziara yake Mkoani Dodoma ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassani ambapo amewataka Mawaziri kufanya ziara katika mikoa yote nchini na kukagua miradi inayotekelezwa na Serikali pamoja na kuangalia thamani ya fedha iliyotumika.

Pichani ni mwonekano wa ndani ya jengo la maabara lililokaguliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Hamadi Masauni