Dodoma FM

Babu adaiwa kumlawiti mjukuu wake na kutoweka

7 October 2024, 7:03 pm

Na Mindi Joseph.

Babu anayedaiwa kumlawiti mjukuu wake wa miaka 12  katika Mtaa Ipagala jijini Dodoma ametoweka nyumbani kwake na hajulikani  alipo baada ya kufanya tukio hilo mwishoni mwa wiki jana.

Mwenyekiti wa mtaa wa Ipagala jijini Dodoma Bw. Elenei Paulo amesema kuwa walipata taarifa hiyo kutoka kwa walimu wa shule anayosoma  binti huyo.

Mwenyekiti wa mtaa wa Ipagala Jijini Dodoma Bwn. Elenei Paulo
Sauti ya Bw. Elenei Paulo

Baadhi ya majirani ambao wanamfahamu kwa ukaribu babu huyo wameshangazwa na kitendo alichofanya mzee huyo . Tukio hilo limetokea mwishoni wa wiki jana na kuzua sintofahamu katika jamii.

Pichani moja ya jirani akieleza kutokea kwa tukio la ulawiti wa binti wa miaka 12
Sauti za wananchi