Dodoma FM

Sagini awapongeza waandishi wa habari

25 September 2024, 8:27 pm

Na Yussuph Hassan

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Jumanne Sagini amepongeza waandishi wa habari kwa kutumia kalamu zao kujenga nchi ,kukosoa pamoja na kuelimisha wakati akifungua semina ya wanahabari ya kusherekea miaka 70 ya Misaada ya Japan.

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Jumanne Sagini
Sauti ya Mhe. Jumanne Sagini

Shirika la Misaada ya Maendeleo Jica limetoa misaada Nchi 190  na Mkoani Dodoma kijiji cha Zuzu kimenufaika kupitia mradi wa ukarabati visima na kuchangia wanakijiji 4250 kunufaika.