Dodoma FM

Dodoma yafurahia wiki ya Madaktari Bingwa

23 September 2024, 8:43 pm

Ujio wa Madaktari Bingwa mkoani Dodoma unatajwa kuwasaidia wananchi kupata huduma za kiafya . Wananchi takribani 100,000 wanatarajia kupata huduma za afya kutoka kwa Madaktari Bingwa kwenye Halmashauri 184 kote nchini.

Na Mindi Joseph.

Jumla ya Madaktari Bingwa na Bobezi wa Rais Samia wapatao 50 watahudumia wananchi kwa siku sita kwenye Halmashauri zote nane za Mkoa wa Dodoma. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyemule amesema kuwa Madaktari hao  watafanya kazi za Kibingwa na Bingwa Bobezi sambamba na kuwajengea uwezo watumishi wa Afya waliopo kwenye ngazi za msingi.

Mhe. Senyemule amesema hayo wakati wa mapokezi wa Madaktari hao leo 23 Septemba 2024 jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyemule
Sauti ya Mhe. Rosemary Senyemule

Aidha  wananchi nao hawakusita kueleza furaha yao kwa ya kupata huduma  za afya kutoka kwa Madaktari bingwa watakaokuwa katika hamashauri mbali mbali  jijini Dodoma.

Sauti za wananchi
Picha kuonesha washiriki wakati wa mapokezi ya Madaktari Bingwa Jijini Dodoma