Migahawa Hombolo yavutia kwa usafi
18 September 2024, 7:42 pm
Wanafunzi kutoka Chuo cha Serikali za Mtaa Hombolo wanasema hali ya usafi kwa baadhi ya watoa huduma ya chakula imeimarika.
Na Mindi Joseph.
Suala la usafi jambo ni muhimu katika kujikinga dhidi magonjwa yasababishwayo na uchafu. Hivyo ni jambo la msingi kila mmoja wetu kuhakikisha kuwa anazingatia tararibu za usafi ikiwemo kunawa mikono kwa maji safi tiririka na sabuni mara kwa mara hasa baada ya matumizi ya maliwato, kabla na baada ya kula hata pia kabla ya kuanza mapishi.
Katika kitongoji cha Hombolo jijini Dododma, ni eneo ambalo limebahatika kuwa na migahawa mingi ambapo wateja wake kwa asilimia kubwa ni wanafunzi kutoka Chuo cha Serikali za Mtaa Hombolo wanasema hali ya usafi kwa baadhi ya watoa huduma ya chakula imeimarika.
Kwa upande wa wauzaji wa chakula Mama Lishe wanasema jukumu lao la kwanza ni kuhakikisha mazingira ya mgahawa yanakuwa safi ili kuwalinda wananchi na magonjwa ya mlipuko..