Dodoma FM

Ally Kamwe apewa kazi PPRA

21 August 2024, 6:14 pm

Picha ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma PPRA Denis Simba akimkabidhi Mwaliko rasmi Meneja wa Mawasiliano na Habari wa klabu ya Yanga Ally Kamwe ofisini kwake ,jijini Dodoma.Picha na Selemani Kodima.

Kongamano la 16 la Ununuzi wa Umma la Afrika Mashariki  limebeba kauli mbiu isemayo  (Matumizi ya Dijitali kwa Ununuzi wa Umma Endelevu) ambapo litahusisha mataifa mbalimbali kutoka ukanda wa afrika mashariki .

Na Selemani Kodima

Kuelekea kufanyika kwa kongamano 16 la ununuzi wa Umma la Afrika Mashariki ,Mamlaka ya Ununuzi wa Umma PPRA  imeendelea kuwakumbusha watanzania kujitokeza katika kongamano hilo litakalofanyika jijini Arusha.

Akizungumza leo mbele ya waandishi wa habari Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Denis Simba  wakati wa zoezi la kumkabidhi  Mkuu wa Mawasiliano na Habari wa Klabu ya Yanga Ally Kamwe Mwaliko na jukumu la kufahamisha umma kuhusu Kongamano hilo ambalo lizinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.

Sauti ya Denis Simba

Kwa upande wake Mkuu wa Mawasiliano wa Yanga Ally Shaban Kamwe akizungumza baada ya kukabidhiwa jukumu amesema haya

Sauti ya Ally Kamwe

Kongamano la 16 la Ununuzi wa Umma la Afrika Mashariki  limebeba kauli mbiu isemayo  (Matumizi ya Dijitali kwa Ununuzi wa Umma Endelevu) ambapo litahusisha mataifa mbalimbali kutoka ukanda wa afrika mashariki .