Dodoma FM

Makamu wa rais kufanya ziara ya siku tatu Dodoma

17 August 2024, 3:58 pm

Picha ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma akielezea kuhusu ziara ya makamu wa rais inayo tarajia kuanza August 19.Picha na Seleman Kodima.

Dkt Philip Mpango ataanza ziara yake mkoani Dodoma tarehe 19 mwezi huu hadi tarehe 21 mwezi nane kwenye wilaya za Chamwino ,Bahi ,Mpwapwa,Kongwa ,chemba na Kondoa.

Na Seleman Kodima.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Dkt. Philip Isdory Mpango anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi katika mkoa wa dodoma yenye lengo la kukagua miradi ya maendeleo.

Akizungumza juu ya Ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amesema kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Mpango ataanza ziara yake mkoani Dodoma tarehe 19 mwezi huu hadi tarehe 21 mwezi nane kwenye wilaya za Chamwino ,Bahi ,Mpwapwa,Kongwa ,chemba na Kondoa.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ameeleza lengo la Ziara hiyo ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika ziara hiyo Makamu wa Rais ataanza kutembelea wilaya ya Chamwino kwa ajili ya kuweka jiwe la Msingi katika kiwanda cha Zabibu.

Aidha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amesema ziara ya Makamu wa Rais itaitimishiwa Wilayani chemba kwa mkutano mkubwa wa wananchi na uzinduzi wa jengo la Halmashauri ya Wilaya hiyo.