Dodoma FM

Wananchi Bahi Sokoni waipongeza serikali kuwasogezea huduma muhimu

13 August 2024, 4:03 pm

Picha ni nguzo ya umeme ambapo tayari eneo hilo lina huduma ya Umeme .Picha na Kadala Komba.

Pamoja na maendeleo makubwa yaliyofanyika kwenye kijiji hicho bado wana uhaba wa huduma ya soko.

Na Kadala Komba.
Wananchi wa Kijiji cha Bahi Sokoni Wilayani Bahi Mkoani Dodoma wameipongeza Serikali kwa hatua ya kuwasogezea huduma muhimu za kijamii ikiwemo maji na umeme katika maeneo yao.
Wananchi hao akiwemo joseph mark, elizabert Jackson pamoja n apaul france wamebainisha hayo wakati wakizungumza na Taswira ya habari Kijiji hapo kuhusu upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii.

Sauti za wananchi.

Kwa upande wake Balozi wa kijiji cha Bahi sokoni mtaa wa Chihona Juma Zizila ambaye amekuwa kiongozi wa kijiji hicho tangu mwaka 1998 kama Balozi anasema pamoja na maendeleo makubwa yaliyofanyika kwenye kijiji chake bado wana uhaba wa huduma ya soko.

Sauti ya Bw.Juma Zizila .