Dodoma FM

Jiji la Dodoma lavunja rekodi ukusanyaji wa mapato ya ndani

8 August 2024, 5:37 pm

Picha ni Mkurugeni mtendaji wa halmashauri ya jiji la Dodoma Bwn. John Kayombo akizungumza katika balaza la madiwani. Picha na Jiji la Dodoma.

Wakazi wa Dodoma wameipongeza halmashauri kwa hatua hiyo.

Na Fred Cheti.
Halamshauri ya jiji la Dodoma imeweza kuvuka lengo la ukusanyaji mapato ya ndani kwa mwaka ulioisha kwa asilimia 103 ambapo ilipanga kukusanya na kunitumia shilingi 123.8 badala yake imeweza kukusanya shilingi bilioni 131.4.

Hayo yamebainishwa na Mkurugeni mtendaji wa halmashauri ya jiji la Dodoma Bwn John Kayombo wakati akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani jijini hapa wakati wa uwasilishaji wa taarifa za kata robo za nne.

Sauti ya Bwn John Kayombo .

Kufuatia mafanikio hayo wakazi wa Dodoma wameipongeza halmashauri kwa hatua hiyo huku wakitarajia mapato hayo kutumika katika maendeleo pamoja na kuongeza wigo wa utoaji mikopo ya asilimia 10 kwa makundi ya vijana,wanawake na wenye ulemavu.

Sauti ya Mkazi wa jiji la Dodoma.