Dodoma FM

DUWASA kuendelea kushirikiana na mamlaka za serikali kufanikisha upatikanaji wa maendeleo

6 August 2024, 6:13 pm

Picha ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Mkoa wa Dodoma (DUWASA ) Mhandisi Aron Joseph.Picha na Seleman Kodima.

Itaendelea kushirikiana na mamlaka za serikali za mitaa katika kuhakikisha wanafanikisha upatikanaji wa maendeleo kwa wananchi.

Na Seleman Kodima.
Katika kuhakikisha wanatekeleza kauli mbiu ya Mwaka huu ya Maonesho ya wakulima na wafugaji Nane nane 2024,Mamlaka ya Maji safi na usafi wa mazingira (DUWASA )imesema itaendelea kushirikiana na mamlaka za serikali za mitaa katika kuhakikisha wanafanikisha upatikanaji wa maendeleo kwa wananchi.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Mkoa wa Dodoma (DUWASA ) Mhandisi Aron Joseph wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna Mamlaka hiyo inavyotumia maonesho ya wakulima na wafugaji Nane nane kutoa Huduma kwa wananchi.

Sauti ya Mhandisi Aron Joseph.