Dodoma FM

Ifahamu ngoma aina ya Mambala inayochezwa na Warangi

6 August 2024, 5:30 pm

Picha ni wenyeji wa kata ya Kingale wakicheza ngoma hiyo inayo fahamika kama Mambala.Picha na Fahari ya Dodoma.

Tunayo ngoma kwaajili ya wanawake ambao hawajaweza kupata watoto walichezewa ngoma ya mambala.

Na Yussuph Hassan.
Yapo mafanikio ambayo watu wa kata ya Kingale wanayafurahia lakini bado hawasahau mila na tamaduni zao ambazo wanazienzi japokuwa kuna maendeleo mengi ya kisayansi na kitekonolojia kwa sababu mila hizo zinaonekana kuwa zinawaletea faida na kutunza utamaduni wao.

Picha ni moja ya nyumba zinazo patikana katika kata hiyo ya Kingale.Picha na Fahari ya Dodoma.

Hapa mwenyeji Ramadhani anatueleza utamaduni wao kwa mwanamke ambaye alikuwa hapati watoto kuwa alikuwa anachezewa ngoma iitwayo MAMBALA.

Waliitwa watu maalumu kwaaji ya kuandaa ngoma hiyo iliyopigwa usiku kucha bila kupumnzika
Hizo nibaadhi ya tamaduni za kirangi karibu mtangazaji kwa kuangalia FAHARI YA DODOMA kwa wakati mwingine