Dodoma FM

Washauriwa kujiunga na vikundi kurahisisha upatikanaji wa mitaji

5 August 2024, 5:29 pm

Picha ni katibu wa itikadi na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma Jawadu Mohamed.Picha na Fred Cheti.

Na Fred Cheti.
Wananchi jijini Dodoma wameshauriwa kujiunga katika vikundi mbalimbali ili kurahisha upatikanaji wa Mitaji kutoka taasisi za fedha ili kujikiwamua kiuchumi kupitia shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo na biashara.

Kauli imetolewa na katibu wa itikadi na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma Jawadu Mohamed wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea maonesho ya nane yanayoendelea kitaifa katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.

Sauti ya Jawadu Mohamed.

Katika hatua nyingine chama hicho kimewataka wananchi kuchangamkia fursa za uwekezaji katika sekta ya kilimo kutokana na serikali ku weka mazingira wezeshi hasa mapinduzi ya kilimo cha kisasa ili kukabiliana na changamoto ya ajira na kuwa na uhakika wa chakula.

Sauti ya Jawadu Mohamed.

Nae mmoja wa wakulima aliyenufaika na Mkopo wa treka kutoka moja ya taasisi aneleza jinsi ambavyo mkopo ulimvvomnufaisha.

Sauti ya mkulima.