Dodoma FM

Ufunguzi wa barabara za ndani Miganga kuwainua wananchi

1 August 2024, 3:00 pm

Picha ni Barabara ya ndani katika mtaa wa Miganga.Picha na George John.

Na Mindi Joseph.
Ufunguzi wa Barabara za ndani zenye urefu wa Mita 8, 10 na 15 katika Mtaa wa Miganga umetajwa kuwa nyezo muhimu ya kuwainua wakazi wa eneo hilo kiuchumi.

Barabara hizi zinawasaidia wananchi katika usafiri na usafirishaji wa bidhaa mbalimbali.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Miganga Ludovick Chogwe anasema mwanzo walikuwa wanakosa barabara za kupita hali iliyosababisha wakazi hao kuchangia fedha kwa ajili ya zoezi la maboresho ya barabara hizo.

Sauti ya Bw. Ludovick Chogwe .
Picha ni Barabara ya ndani katika mtaa wa Miganga.Picha na George John.

Kwa upande wao wananchi wamepongeza hatua hiyo huku wakiomba maeneo yote ya mtaa kufikiwa na maboresho hayo.

Sauti za Wananchi.

Mtaa wa Miganga una Wakazi zaidi ya 7000 na ufunguzi wa barabara hiyo unatarajiwa kusaidia kuinua uchumi kwa wananchi hao.